Raia wawili wa kigeni wamekamatwa jijini Dar es Salaam kwa kosa la kuishi nchini bila vibali na kuwa watumishi wa serikali.

Msumule: Mkuu wa idara ya uamiaji kanda ya Dar es salaam akitoa taarifa juu ya kukamatwa kwa raia hao wa kigeni.
John Msumule: Mkuu wa idara ya uamiaji kanda ya Dar es salaam akitoa taarifa juu ya kukamatwa kwa raia hao wa kigeni.

Mkuu wa idara ya uamiaji kanda ya Dar es Salaam, John Msumule amesema kwamba raia hao ni Bihalanya Milangita maarufu kwa jina la Roy Bilangita raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Dkt. Ester Mwenitumba raia wa Malawi.

Bw. Msumule amesema Milangita ambaye ni raia kutoka Congo anatuhumiwa kuingia nchini mwaka 1986 na kufanya kazi katika Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kinyume na sheria huku Dkt. Ester Mwenitumba raia wa  Malawi alikuwa mganga mkuu katika kituo cha afya cha Mburahati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *