Raia wa Rwanda wanatarajia kupiga kura kwa ajili ya kumchagua rais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika leo.

Uchaguzi huo utashirikisha wagombea watatu ambao ni Rais wa sasa Paul Kagame, Frank Habineza wa chama cha Green Party na Philippe Mpayimana ambaye ni mgombea binafsi.

Lakini wapinzani hao wote hawatarajiwi kumpa ushindani mkubwa Kagame ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2000.

Uungwaji mkono mkubwa anaopata ndani ya Rwanda rais Kagame unamhakikishia ushindi mkubwa kwenye uchaguzi huo.

Wagombea wengine wanasema wafuasi wao wamenyanyaswa lakini chama tawala kina kana tuhuma hizo.

Katiba ya Rwanda ilirekebishwa mnamo mwaka 2015, na kumpa rais Kagame nafasi ya kushinda muhula mwingine wa miaka 7 na mihula mingine miwili ya ziada ya miaka mitano kila mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *