Raia wa Kenya wanapiga kura kumchagu rais wa nchi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano kwenye uchaguzi mkuu unaofanyika leo.

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa mapema asubuhi kwa ajili ya uchaguzi huo uliojaa upinzani mkubwa kutokana na wagombea kwenye uchaguzi huo.

Upinzani upo kati ya rais wa sasa Uhuru Kenyatta anayetetea kiti chake pamoja na mgombea wa upinzani wa muungano wa NASA, Raila Odinga.

Hapo jana nchi hiyo ilionekana kuwa kimya sana kutokana na wananchi kujiandaa na uchaguzi wa leo ambapo raia wengi wamekuwa na wasiwasi kutokana uchuguzi kuwa na vitisho sana miongoni mwa wagombea.

Matokeo ya uchaguzi huo yatatolewa baada ya kumalizika kwa zoezi la uhesabuji wa kura katika kaunti zote za nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *