Raia wa Gabon leo wanapiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi mkuu.

Wagombezi wakuu ni rais aliye maamlakani Ali Bongo na mpinzani wake mkuu, Jean Ping ambaye alikuwa kiongozi wa zamani wa tume ya umoja wa Afrika.

Rais Bongo alichukua wadhfa wa urais mwaka 2009 baada ya kifo cha babake aliyekuwa rais wa Gabon Omar Bongo.

Rais Bongo ana nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo kwani anadhibiti serikali huku mshindi anahitaji kumzidi mpinzani wake kwa kura moja pekee.

Hata hivyo upinzani umelezea wasiwasi kwamba serikali tayari ‘imetayarisha matokeo kabla ya upigaji wa kura hizo.

Bwana Ping ana uhusiano wa karibu na familia ya Bongo kwani kwa wakati mmoja alikuwa shemeji yake rais Ali Bongo baada ya kumwoa dadake.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon alitoa wito kwa pande zote mbili kudumisha amani kabla na baada ya uchaguzi.

Bwana Ping anaungwa mkono na vigogo wawili wa upinzani ambao pia walikuwa washirika wa karibu wa familia ya Bongo ambao ni Casimir Oye Mba waziri mkuu wa zamani na aliyekuwa spika wa bunge Guy Nzouba Ndama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *