Aliyekuwa mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage ameitaka klabu ya Simba kutopokea kiasi cha fedha shilingi milioni 50 kutoka kwa Yanga baada kushinda kesi dhidi ya beki Hassani Kessy.

Rage ameitaka Simba wapeleke mbele malalamiko hayo kwa shirikisho la soka la kimataifa FIFA kutokana na Yanga kukiukwa mkataba wa beki huyo aliyeingia na klabu ya Simba kabla ajajinga na wana jangwani hao.

Kauli hiyo ya Rage inakuja baada ya kamati ya TFF ya katiba na sheria na hadhi za wachezaji kuitaka klabu ya Yanga kuilipa shilingi milioni 50 kama fidia kwa kitendo cha kumtumia beki Hassan Kessy wakati anamkataba na Simb.

Mwenyekiti huyo wa zamani wa Simba ameitaka timu yake hiyo kutopokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Yanga na badala yake waende mbele zaidi kupeleka malalamiko yao hayo kwa shirikisho la soka duniani Fifa.

Yanga walifanya makosa ya kumsajili aliyekuwa beki wa Simba Hassan Kessy wakati bado mkataba wake ulikuwa ujamalizika na wanamsimbazi hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *