Malkia wa Uingereza, Queen Elizabeth amekosa kuhudhuria ibada ya mwaka mpya katika kanisa la Sandringham kutokana na kuugua homa kali.

Hiyo inakuwa ibada ya pili kuokosa Malikia Elizabeth  baada ya kukosa ibada ya siku kuu ya Krismasi nyumbani kwake Norfolk na hajaonekana hadharani kwa siku 12 sasa.

Msemaji wa Kasri la Buckingham amesema kuwa malkia anaendelea kupata nafuu na hali yake kwasasa ipo vizuri.

Malikia na Duke wa Edinburgh walichelewa kwa likizo yao ya Krismasi kwa siku moja mnamo Disemba 22, na kusafiri kwa kutumia ndege aina ya helikopta badala ya treni kutokana na homa.

Binti Mfalme Anne aliulizwa vile mamake alivyokuwa akiendelea alipowasili katika kanisa ambapo alijibu anaendelea vyema.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *