Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Queen Darleen amefunguka kuhusu ndoa yake na mfanyabiashara Isihaka Mtoro.

Queen Darleen anakiri kuwa hana uhakika kama bado yuko kwenye ndoa au tayari ameachika kutokana na kutokuwa na maelewano kati ya wawili hao.

Anasema kuwa bado anampenda mume wake na huwa wanawasiliana mara kwa mara “Kiukweli mpaka sasa sijijui.

Pia amesema kuwa “Sijui kama nipo kwenye ndoa au sipo kwenye ndoa Nampenda sana mume wangu, Popote alipo ajue kwamba nampenda sana. Yeye ndiye anajua kama nipo naye au sipo naye,” anasema Darleen kwa huzuni.

Kauli hiyo ya Darleen inakuja miezi kadhaa baada ya tetesi kuzagaa kuwa wanga wamepita na ndoa yake baada ya kujaliwa kupata mtoto mmoja na mfanyabiashara huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *