Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Q Jay amsema kuwa mwakani anarudi kamili kwenye anga ya muziki huo baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kutokana na kuokoka.

Q Jay kwa mara ya kwanza tangu arudie Bongo Fleva baada ya kuwa ameokoka, amefungukia projekti yao ya kundi lao la Wakali kwanza kuwa imeshakamilika na mwezi wa kwanza wanarudi rasmi.

Mkali huyo ambaye kwa sasa anaunda Kundi la Busy Boy akiwa na D Malick amesema kuwa, kwa muda mrefu amepitia maisha magumu yaliyomfanya kupotea katika muziki.

Kundi la Wakali Kwanza lilikuwa linaundwa na wakali kama vile Makamua Joslin na Q Jay ambao walijizolea umaarufu kutokana na nyimbo zao kubamba watu miaka ya nyuma.

Q Jay amezungumza stori ya kusikitisha kutokana na kilichomtokea katika maisha yake hadi kushindwa kuimba muziki na kukimbilia jijini Mwanza.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *