Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Q Chief amefunguka na kusema kuwa haikuwa jambo dogo na jepesi kufanya collabo na msanii Patoranking kutoka nchini Nigeria.

Chillah amedai kuwa pesa nyingi zimetumika kufanikisha collabo hiyo kiasi cha kufanya hata mpango wake wa kuoa usogee mbele.

 

Mkali huyo amesema kuwa pesa za kutosha zilitumika jambo ambalo limefanya ashindwe kutimiza ahadi yake aliyowahi kuitoa kuwa ataoa siku za karibuni.

 

Pia ameendelea kusema kuwa anamshukuru sana Qs Mhonda kwani alisimamia jambo hilo mpaka kukamilika japokuwa pesa ya kutosha imetumika kukamilisha kazi hyo.

 

Q Chilla amesema kazi yake na mkali huyo kutoka Nigeria itaachiwa kwenye vituo vya radio na TV baada ya kukamilika kabisa huku akiwataka mashabiki wake kuisubili kwa hamu nyimbo hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *