Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Q Chillah amemalizana na aliyekuwa meneja wake QS Mhonda baada yakukubaliana kuvunja mkataba wa maisha waliokuwa wameingia baina yao.

Q Chilla ameonekana mwenye furaha kubwa baada ya kupokea taarifa ya kuruhusiwa kutoka ndani ya QS J Mhonda.

Baadhi ya maneno aliyoandika Q Chief katika barua yake ambayo imekwenda kwa Muhonda.

Q Chillah asema kilichompelekea yeye kuandika barua hiyo ni kutaka kumshukuru aliyekuwa muajiri wake kwa mema na mazuri yote aliyomfanyia pindi alipokuwa katika kampuni hiyo.

Kwa upande mwingne msanii huyo hakutaka kuzungumza lolote kuhusiana na tetesi zilizoenea kuwa Mb Dogg nae pia ametoka katika Lebo ya QS J Muhonda na kutaka swali hilo atafutwe mwenyewe aweze kufafanua sababu za kuondoka.

Q Chilla amesema kuwa kila mtu anatoka katika kampuni hiyo ana sababu zake binafsi hawawezi wote wakawa sawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *