Staa mkongwe wa Bongo fleva, Q-Chillah amesema hafanyi collabo na wanamuziki wa ndani kwasasa kutokana na soko lake kuangalia kimataifa zaidi.

Mkali huyo amesema kuwa hakufanya kolabo na wasanii waliosainiwa kwenye lebo moja ya QS kwa sababu hakwenda pale kwa sababu ya kufanya kolabo na wasanii hao.

Q Chila amesema kwa sasa anafanya collabo na wasanii wa nje zaidi ili kuweza kutambulika kimataifa zaidi na hasa kwa nchi za Afrika kwa kuwa hapa Tanzania hata akifanya kolabo na wasanii wa hapa ataambiwa anabebwa kimuziki.

Hata hivyo Chillah alimalizia kwa kusema kuwa kwa sasa ana mpango wa kufanya kolabo na msanii  nguli wa bongo fleva Solo kwa kuwa yupo Tanzania na ni mtu anayeamini kwamba wakifanya kolabo la pamoja litakuwa poa sana.

Q Chilla ni mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na kazi zake kukubalika kila eneo la ndani na nje ya Tanzania.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *