Rais Vladimir Putin wa Urusi ametuma salamu za rambirambi baada ya ndege ya kivita ya Urusi kuwaua kwa bahati mbaya wanajeshi watatu wa Uturuki kaskazini mwa Syria.

Wanajeshi hao ambao walikuwa wanawaunga mkono waasi wa Syria katika jitihada za kuuteka mji wa al-Bab kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State.

Urusi na Uturuki ambazo zinaunga mkono pande hasimu kwenye mgogoro wa Syria, hivi karibuni zimekuwa zikiungana mkono kwenye mapambano dhidi ya mashambulizi ya IS.

Jeshi la Uturuki limedai kuwa ndege ya Urusi ilishambulia jengo ambamo baadhi ya wanajeshi wake walikuwemo na kupelekea mauaji hayo.

Ikulu ya Kremlin imedai kuwa rais Putin alimpigia simu rais wa Uturuki na kuelezea masikitiko yake kutokana na ajali hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *