Staa wa kundi la Psquare, Peter Okoye kutoka Nigeria ameomba msamaha kwa mashabiki wake kufuatia ugomvi na kaka yake Paul Okoye ambaye wanaunda kundi hilo maarufu barani Afrika.

Kupitia video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii Peter Okoye amesema timu nzima ya Psquare kwa sasa imerudi tena pamoja na kufanya kazi kama zamani chini ya kaka yao Jude Okoye.

Peter alikuwa na uhasama na pacha wake Paul, ambaye ndiye amekuwa akiimba naye kwa zaidi ya miaka kumi hali iliyofanya kugawa kundi hilo.

Peter na Paul ambao wanaunda kundi la Psquare wametoa nyimbo nyingi zilizovuma ndani ya Nigeria na nchi nyingine za Afrika pamoja na dunia kwa ujumla kama vile Ifunanya, No One Like You na Beatfully Unyinye waliyomshirikisha Rick Ross.

Psquare: Wakiwa pamoja na kaka yao Jude Okoye.
Psquare: wakiwa pamoja na kaka yao.

PETER

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *