Klabu ya Paris Saint – German imeifunga Barcelona 4-0 kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza wa 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika uwanja wa Parc de Princes nchini Ufaransa.

Kiungo wa PSG, Angel Dimaria amefunga magoli mawili katika dakika ya 18 na 55 huku magoli mengine yakifungwa na Julian Draxer mnamo dakika ya 40 na goli la mwisho likifungwa na Edson Cavani katika dakika ya 71.

Barcelona walionekana kuzidiwa sana katika mchezo huo mpaka kushindwa kupata hata goli moja kwenye mechi hiyo.

Mchezo mwingine uliwakutanisha Benfica ya Ureno na Borrusia Dortmund na mpaka mchezo unamalizika Benfica wameshinda 1-0 kwenye mechi hiyo iliyofanyika Ureno.

Mechi za marudiano zitafanyika baada ya wiki moja huku maswali yakiwa je Barcelona anaweza kulipiza kisasi na kuvuka hatua ya robo fainalia ya kombe hilo.

Mechi nyingine zinatarajiwa kuchezwa leo katika viwanja viwili tofauti uku Bayern Munich ya Ujerumani akiwa mwenyewe wa Arsenal ya Uingereza na Real Madrid akimkaribisha katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *