Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) wameafikiana dili la kumsajili kwa mkopo mshambuliji w Monaco, Kylian Mbappe.

Kinda huyo anatarajiwa kuondoka AS Monaco kwa mkopo wa mwaka mmoja, utakaogharimu kiasi cha Euro milioni 166.

Mbappe mwenye umri wa miaka 18 aliachwa kwenye benchi wakati wa mchezo wa ligi ya nchini Ufaransa hapo jana dhidi ya Olympic Marseille ambapo Monaco walishinda 6-1.

Mshambuliaji huyo wa kifaransa, amecheza mchezo mmoja tangu msimu wa 2017/18 ulipoanza, na sababu kubwa iliyomzuia kutokua sehemu ya kikosi katika michezo miwili iliyopita.

Mbappe amekua akihusishwa na mpango wa kuondoka Stade Louis II tangu mwishoni mwa msimu uliopita, na klabu kadhaa ikiwepo Real Madrid, Manchester United, Manchester City, Arsenal na FC Barcelona zilitajwa kuwa katika mawindo ya kumuwania.

Hata hivyo taarifa za awali zinaeleza kuwa, ushawishi mkubwa wa usajili wa Mbappe kuelekea mjini Paris, umechagizwa na uwepo wa mshambuliaji kutoka nchini Brazil Neymar aliyesajiliwa mapema mwezi huu, akitokea FC Barcelona kwa ada iliyoweka rekodi duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *