Promota mkongwe, Bob Arum ametabiri kuwa bingwa wa dunia wa masumbwi ya uzito wa juu, Anthony Joshua atapokea kipigo chake cha kwanza, Aprili Mosi mwaka huu, kutoka kwa Joseph Parker.

Bob Arum ambaye ameendelea kupromoti mapambano yake kupitia Top Rank, amesema amemueleza kila mtu namna ambavyo Joshua atapigwa kwa mara ya kwanza na kwamba hilo litadhihirika usiku wa pambano.

Amesema kuwa “Parker atampiga Joshua. Ninamwambia kila mtu, Parker atambomoa. Kila mtu anasema Joshua ni bondia mzuri, achana na hilo. Parker ni bondia mzuri zaidi yake na atampiga kuanzia raundi ya 4 hadi katikati ya raundi ya 12,”.

Hata hivyo, Joshua ametamba kuwa atampasua Parker na kwamba atakuwa mhanga wa mwisho wa kipigo cha KO kutoka kwake.

Amesema kuwa ingawa anajua Parker amefanya maandalizi mazuri, yeye amefanya maandalizi mazuri zaidi yake na kwamba atahakikisha anamzimisha kati ya raundi ya sita hadi ya nane.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *