Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu staa wa Hip-Hop nchini, Pofessor Jay anatarajia kuachia video mpya ya wimbo wake unaokwenda kwa jina la “Kazi Kazi” aliyomshirikisha mwanamuziki wa nyimbo za kisingeli, Sholo Mwamba.

Staa huyo ambaye kwasasa ni mbunge wa jimbo la Mikumi mkoani Morogoro kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema wameanza kushoot video hiyo maeneo ya Manzese uwanja wa fisi kwa hiyo mashabiki wake wakae mkao wa kula baada ya kimya kingi.

Video ya wimbo huo unaongozwa na muongozaji Traveller huku audio ikitengenezwa na Mesen Selekta.

Pofessor Jay: Akiimba Moja ya shoo zake
Pofessor Jay: Akiimba Moja ya shoo zake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *