Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameitaka Bodi mpya ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kusimamia Menejimenti ya Mamlaka hiyo katika Idara ya Utawala na Rasilimali na kuhakikisha ajira zote zinazotolewa zinazingatia sifa na vigezo vya kuajiri..

Profesa Mbarawa amesisitiza bodi hiyo kuifanyia kazi Ripoti ya Uchunguzi wa uendeshaji wa viwanja hivyo nchini na kufanya mabadiliko mara moja.

Pia Profesa Mbarawa ameitaka Bodi hiyo kusimamia kwa uadilifu miundombinu yote ya viwanja vya ndege nchini na kuhakikisha mashine za ukaguzi zinafanya kazi saa 24 ili kudhibiti mianya yote ya rushwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Ninatubu Lema amemhakikishia Waziri huyo kuwa ataongeza ushirikiano na wafanyakazi wote na kusimamia maagizo yote yaliyotolewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *