Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema kuwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha alikuwa sahihi kufuta matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar kwasababu Maalim Seif alifanya kosa kujitangazia ushindi.

Profesa Lipumba amesema hayo leo katika mahojiano na kituo cha runinga cha Clouds Tv kwenye kipindi cha Clouds 360 ambapo ana jibu hoja za Maalim Seif aliyehojiwa kwenye kipindi hicho jana.

Katika mahojiano hayo, Lipumba amesema kuwa sababu ya kujiuzuru kama Mwenyekiti wa Chama hicho ni sintofahamu katika umoja wa UKAWA kumchagua Edward Lowassa kugombea urais kupitia umoja huo.

Lipumba amesema kuwa hakupenda Lowassa agombee urais kupitia umoja huo kwasababu ni mzigo kumnadi kutokana na kashfa yake.

Mwenyekiti huyo anayetambuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa amesema kuwa kabla ya umoja huo kumkaribisha Lowassa walijua mgombea urais atakuwa ni Dkt. Wilbroad Slaa lakini ni tofauti.

Kuhusu kutumika na CCM kuibomoa CUF, Lipumba amesema si kweli habari hizo yeye ni mpinzani na ataendelea kusimamia misimamo yake ndani ya CUF na si vinginevyo.

Jana katika mahojiano ya Maalim Seif alisema kuwa watu wote wanaompinga ndani ya CUF wanatumwa na CCM kukibomoa chama hicho akiwemo, Profesa Lipumba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *