Mwanamuziki mkongwe na mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ amesema kuwa anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake Grace mwakani kabla ya kufika mwezi wa sita.

 

Profesa Jay amesema hayo baada ya mashabiki wake kumuuliza maswali lini wawili hao watafunga ndoa baada ya kudumu kwenye mahusiano kwa muda mrefu na mpenzi wake huyo.

 

Mbunge huyo amesema hayo leo kutokana na siku yake kuzaliwa ambapo ametimiza umri wa miaka 41.

 

professor-jay-and-fiancee-august-2014-bongotoday-com-bt-01

Pia Prof Jay ametumia nafasi hiyo kuwashukuru mashabiki wake katika muziki, pamoja na wananchi jimbo la Mikumi kwa sapoti kubwa wanayompa huku akiahidi kuendelea kuwatumikia bila ubaguzi wowote.

 

Katika hatua nyingine Prof Jay amemzungumzia mkulima mmoja wa jimboni kwake aliyejeruhiwa kwa kupigwa mkuki mdomoni hivi karibuni na kusema kuwa hali yake inaendelea vizuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *