Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Joseph Haule A.K.A Profesa Jay kupitia akaunti yake Instagram leo amewajulisha mashabiki zake siku ya Jumatano Machi 15 ataachia wimbo mpya.

Kupitia akaunti yake hiyo Profesa Jay amesema kuwa siku hiyo ataachia audio pamoja na video ambapo utaanza kupigwa katika media mbali mbali.

Jay ameandika maneno yafuatayo kupitia ukurasa wake huo  “The Wait is Over….Jumatano Tar 15 March Naangusha MZIGO MPYA kwa watu wangu wa nguvu.#KIBABE (The ICON) Stay tuned on your favourite Radio and TV stations ,”

Nyimbo ya mwisho kuachia mkali huyo ilikuwa ‘Kazi Kazi’ aliyoimba kwa mahadhi ya Singeli aliyomshikisha Sholo Mwamba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *