Nguli wa muziki wa hip hop nchini, Joseph Haule A.K.A Prof Jay amewataka wasanii wa singeli kukomaa katika muziki huo  ili waweze kuufikisha mbali na siyo kubweteka kusubiri watu wengine kuwanyanyua kwenye muziki huo.

Profesa Jay ambaye ni mbunge wa Mikumi mkoani Morogoro amesema yeye hana mpango wa kuendelea kuimba muziki huo na kwamba alijitoa kufanya  wimbo mmoja ili kuonesha vipaji vilivyopo kwenye muziki huo ikiwa ni pamoja na  kuupa hadhi kwenye jamii ili uweze kupata heshima.

Pia Jay ameongeza kwa kusema nyimbo za kiharakati zilimpelekea kuwa Mbunge kabla ya kuingia Bungeni kwa kuwa kila wimbo ambao aliokuwa anaufanya ulikuwa unabeba shida za wananchi kiuhalisia na kuendelea kusema kuwa hawezi kubadilika.

Vile vile Profesa amewataka  wasanii  kutoridhika  na pesa kidogo wanazopatiwa kwenye show za nje ya nchi bali waongeze juhudi ili kuufanya muziki ufike mbali zaidi ya hapa ulipofikishwa huku akiweka wazi mpango wake wa kuachia albam mpya hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *