Mbunge wa Jimbo la Mikumi mkoani Morogoro na Mkali wa Hip Hop na mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule (Profesa Jay) amemvisha pete ya uchumba mpenzi wake Grace Mgonjo ambaye ni mzazi mwenzie.

Prof Jay mwishoni mwa mwaka uliopita aliahidi na kusema kuwa haitapita muda mrefu sana watu wataanza kupewa kadi kwa ajili ya ndoa yake.

“Asante sana Mungu, leo tunaufunga mwaka namna hii na Mke wa Profjize” aliandika Prof Jay katika picha akiwa anamvisha pete ya uchumba Grace Mgonjo.

Mbunge huyo ametumia nafasi hiyo kwa ajili ya kuukaribisha mwaka akiwa tayari ameshamvalisha pete mpenzi wake kinachosubiliwa na ndoa tu kwasasa ambapo siku si nyingi jamba hili litafanyika.

Profesa Jay ataungana na wanamuziki wenzake waliofunga ndoa mwaka jana ambao ni Tunda Man, Mabeste pamoja na Nyandu Tozy.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *