Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Profesa Jay amemshangaa waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Mwakyembe kuwataka wasanii kuacha kuimba nyimbo za siasa.

 

Kauli hiyo ya Profesa Jay imekuja kufuatia waziri Mwakyembe kuongea Bungeni na kuwataka wasanii wa Tanzania kuacha kuimba nyimbo zenye jumbe za siasa kwani hawatafanikiwa.

 

Waziri Mwakyembe aliwashauri wasanii kuachana na nyimbo za siasa kwani hawatafanikiwa kwakuwa hakuna msanii ambaye alijikita katika kuimba siasa na akafanikiwa.


Profesa Jay ambaye ni Mbunge wa Mikumi amesema kuwa haiwezekani kuwachagulia wasanii mambo ya kuimba kutokana siasa ni maisha kwa hiyo hawawezi kuacha kuimba.

 

Mbunge huyo amesema kuwa hata yeye tungo zake nyingi zilikuwa zinaegemea kwenye siasa kama vile ndiyo mzee, siyo mzee na ndiyo zilizomtambulisha kwenye muziki kutokana na mashabiki kutopenda kusikiliza nyimbo za mapenzi.

 

Profesa Jay ameongeza kwa kusema kuwa kuwaambia wasanii waimbe nyimbo za maisha yao tu na washindwe kuimba vitu vingine, maana yake unataka kutoa ‘green light’ kwa wasanii sasa waanze kuimba mambo ya mapenzi.

 

Mbunge huyo alidai kuwa wapo wasanii walioimba kuhusu siasa na masuala ya kijamii kama 2Pac, BIG, Bob Marley, Lucky Dube na wengine ambao walisaidia dunia kuhama katika ngazi moja kijamii hadi ngazi nyingine.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *