Mwanamuziki wa hip hop, Joseph Haule (Profesa Jay) amesema hana kinyongo na wasanii wote na wote waliokwenda jimboni kwake kipindi cha uchaguzi kwa ajili ya kumpinga.

Profesa Jay ambaye ni mbunge wa Mikumi amesema hayo kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika kwa kuandika maneno machache yanawagusa moja kwa moja wasanii wenzake waliokuwa nje ya chama hicho kuwa amewasamehe ila amewataka wajiongeze kwa maana sanaa inahitaji umoja.

 Ameandika kama ifuatavyo “Nilishawasemehe wasanii wenzangu waliokuja jimboni kupinga Ubunge wangu mabasi kwa mabasi,  jiongezeni wanangu. Asante wana Mikumi kwa kuwa na imani kwangu, sanaa yataka umoja nitakubeba ukianguka”.

Kwa upande mwingine msanii huyo amewataka mashabiki na wapenzi wa muziki wake wakae tayari kupokea mzigo mpya siku ya kesho Jumatano unaotarajiwa kupewa jina la ‘kibabe’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *