Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Profesa Jay amefanya sherehe ya ndoa yake kwa mara ya pili jimboni kwake Mikumi mkoani Morogoro.

Sherehe ya kwanza ya ndoa yake alifanya katika Ukumbi wa Mlimani City, siku aliyofunga ndoa, sherehe ambayo ilihudhuriwa na viongozi wengi maarufu wakiwemo Edward Lowassa, viongozi wa serikali, wananii na watu mbalimbali.

Siku chache baadaye alisafiri na kwenda Jimboni kwake Mikumi mkoani Morogoro ambako pia alifanya sherehe nyingine.

Akizungumza na wananchi wa Mikumi, Prof. Jay amefunguka kisa cha yeye kufanya maamuzi hayo ya kufanya sherehe mara mbili ni kuwashukuru wananchi wa jimbo la Mikumi kwa kumchagua.

Profesa Jay alifunga ndoa July 9, na mpenzi wake wa siku nyini, Bi. Grace katika Kanisa la Mt. Joseph lililopo Posta ya Zamani jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *