Waziri wa Elimu, Sayansi na Teckonolojia, Profesa Joice Ndalichako anatarajiwa kufungua kongamano la tano la Sayansi na Teknolojia na ubunifu linaloandaliwa na Tume ya taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) litakalofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi huu.

Mkurugenzi wa COSTECH, Dkt Hassan Mshinda
Mkurugenzi wa COSTECH, Dkt Hassan Mshinda

Mkurugenzi wa COSTECH, Dkt. Hassan Mshinda amesema kongamano hilo litakuwa la siku tatu litawakutanisha watafiti, wanasayansi na wabunifu ambapo uwasilishaji wa matokeo ya utafiti mbalimbali na maonesho ya kazi za kisayansi na ubunifu vitakuwa sehemu kubwa ya kongamano hilo.

Mkurugenzi huyo amesema kwamba dhima ya kongamano hilo ni utafiti wenye msukumo wa kibiashara ni kichocheo kuelekea ukuzaji na maendeleo ya viwanda ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano ya kukuza uchumi wa taifa.

Katika kongamano hilo pia watafiti waliobobea katika taaluma, wabunifu, watunga sera na wadau wengine mbalmbali kutoka sekta za umma na binafsi watajadili kwa kina na kutoa majibu ya namna sayansi, teknolijia na ubunifu vinavyoweza kukuza maendeleo ya viwanda kwa kasi zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *