Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu, Profesa Norman Sigalla amekitaka chuo cha Usafirishaji (NIT) kuboresha idara ya ukaguzi wa magari kwa ajili ya kukijengea uwezo wa kufanya kazi hiyo.

Profesa Sigalla amesema hayo baada ya kamati hiyo kusikiliza na kujadili taarifa ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuhusu utendaji kazi wa NIT na Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI).

Sigalla ameitaka wizara ya Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasilano kusimamia maboresho ya miundombinu kwenye vyuo vya NIT na DMI ili viwe na hadhi kulingana na umuhimu wake kwa taifa.

Pia ametoa changamoto kwa vyuo hivyo vijikite kwenye utafiti na kutoa machapisho yenye lengo la kutatua matatizo yanayolikabili taifa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *