Katibu mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo amewaaka wapinzani kumuunga mkono Rais Magufuli kwenye sakata la usafirishaji wa mchanga wa madini.

Kauli hiyo ameitoa jana baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kupokea ripoti ya pili kuhusu usafrishaji wa mchanga wa madini (Makinikia).

Profesa Mkumbo amesema kuwa wapinzani wa Tanzania wanaugua ugonjwa wa kupinga kila kitu na kwamba wanatakiwa kumuunga mkono rais Magufuli kuokana na sakata la mchanga. kijamii.

Pro. Mkumbo ametoa maoni hayo kupitia akuanti yake ya mtandao wa kijamii ambapo amewataka watanzania kwa ujumla kumuunga mkono Rais Magufuli kwenye vita hii ya uchumi dhidi ya rasilimali za taifa.

Ikumbukwe kuwa kabla ya uteuzi wa kuwa katibu mkuu wa wizara ya Maji, Profesa Mkumbo alikuwa mwanasheria wa chama cha ACT-Wazalendo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *