Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo ameweka wazi sababu ya yeye kukubali kuteuliwa kushika wadhifa huo, licha ya misimamo ambayo alikuwa nayo awali dhidi ya wasomi wanaoteuliwa kushika wadhifa mkubwa serikalini.

Prof. Mkumbo amesema kilichofanyika kwake ni kupandishwa cheo kutoka nafasi aliyokuwa nayo awali, na asingeweza kukataa kwani ni heshima kubwa aliyopewa na Rais.

Prof. Mkumbo ameendelea kwa kusema kwamba baada ya kuteuliwa huko hakuchelewa kuachia wadhifa ambao alikuwa nao kwenye chama cha ACT- Wazalendo, kwa kuwa aliona dhahiri asingeweza kuendeleza harakati alizokuwa anafanya kwenye chama.

Amesema kuwa “Katika nafasi ya Katibu mkuu, mimi sio tu mtumishi wa umma, mimi ni serikali nawajibika kwa serikali kuisimamia, kutekeleza mipango ya serikali, tofauti kabisa na uhadhiri, kwenye chama nilikuwa nafanya harakati, nikaona hili sasa haliwezekani, ikabidi niwaombe wenzangu kwamba hapa nilipofika majukumu haya siwezi kuchanganya na uanachama wangu, ikabidi niweke uanachama pembeni”,.

Hivi karibuni Kitila Mkumbo amejiondoa unachama wa ACT- Wazalendo, akisema kwamba hatoweza kutumikia serikali akiwa mwananchama wa chama hicho, kwani kuna mgongano wa maslahi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *