Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua Prof. Yunus Mgaya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).

Taarifa ya Ikulu jijini Dar es Salaam imesema uteuzi wa Prof. Mgaya unaanza mara moja.

Prof. Mgaya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Mwele Malecela ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *