Waziri wa Uejenzi, Uchukuzi na Mawasilano, Prof. Makame Mbarawa ameto wiki mbili kwa mkandarasi  wa kampuni ya Chongqing International Construction Corporation (CICO) kutoka China anayejenga barabara ya Tabora- Sikonge yenye urefu wa kilomita 30 kuongeza vifaa vya ujenzi katika eneo la mradi huo.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo na kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wake Prof. Mbarawa amemtaka mkandarasi huyo kutumia kipindi cha muda wa ziada cha utekelezaji wa mradi huo kilichoongezwa kukamilisha.

Pia Mbarawa amesema kuwa ujenzi wa mradi huo uende sambamba na viwango bora vya barabara vilivyomo kwenye mkataba uliosainiwa.

Vile vile waziri Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara Tabora- Nyahua yenye urefu wa kilomita 85 kipande cha barabara ya Tabora mjini chenye urefu wa kilomita 6 kinachojengwa na kampuni ya Chongqing Foreign Trade and Economic Cooperation kutoka China na kumtaka mkandarasi kukamilisha barabara hiyo ifikapo Disemba mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *