Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amefanya mabadilko katika mradi wa ujenzi wa jengo la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Profesa Mbarawa ameteua jopo la wahandisi saba kwa ajili ya kusimamia maendeleo ya ujenzi wa mradi huo unaendelea katika uwanja wa ndege huo.

Waziri huyo amesema kuwa ujenzi wa jengo jipya la Uwanja huo (Terminal Three) unaendelea baada ya mabadiliko hayo na kwamba hakuna tena mgomo kwani mkandarasi aliyetishia kusimamisha ujenzi atalipwa fedha zake mapema kama alivyoahidiwa jana na Rais Magufuli katika ziara yake.

Awali mkandarasi anayejenga uwanja huo ambaye ni kampuni ya BAM International alitangaza kususia kuendelea na ujenzi huo kutokana na kutolipwa kiasi cha shiilingi bilioni 23 ambacho serikali imeahidi kukilipa haraka.

Mabadiliko hayo yamekuja kufuatia ziara aliyofanya Rais Magufuli katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam na kugundua mapungufu mengi kwenye ujenzi hu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *