Mwenyekiti wa (CUF), Profesa Lipumba amesema kuwa Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad ana amewaponza wabunge nane waliovuliwa uanachama wa CUF

Profesa Lipumba amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kusema Katibu Mkuu wa (CUF)  Maalim Seif na yeye anayake ya kujibu mbele za Kamati ya Maadili na Nidhamu ya CUF.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa CUF Taifa  Maalim Seif Sharif Hamad amesema mpaka sasa wabunge wote nane ambao wanasemakama wamefukuzwa uanachama wameamua kufungua kesi Mahakama Kuu kupinga maamuzi feki ambayo yamefanywa na Baraza Kuu feki na kuitaka Mahakama itamke kuwa wao ni wanachama halali wa CUF na wabunge halali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini pia Katibu Mkuu amesema kuwa Baraza Kuu halali la CUF litakutana kwa dharura siku ya kesho Ijumaa tarehe 28/07/2017 kujadili mambo mbalimbali ambayo yanaendelea katika chama hicho na kutangaza hatua ambazo zitafuata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *