Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi ametajwa katika orodha ya watumishi ambao vyeti vyao vina matatizo.

Uhakiki wa Profesa Kabudi ulifanyika wakati akiwa mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kabla ya kuteuliwa kuwa mbunge na kisha waziri wa Katiba na Sheria.

Waziri Prof. Kabudi ambaye amebobea katika sheria, pamoja na waafanyakazi wengine wa UDSM wametajwa katika orodha ya watumishi wa umma ambao vyeti vyao havijakamilika.

Akizungumza suala hilo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Mukandala alisema kwa Prof. Kabudi ametajwa katika orodha hiyo kwa sababu cheti chake cha kidato cha nne hakikuonekana wakati wa uhakiki.

Aidha, Prof. Mukandala amesema kuwa tayari Prof. Kabudi ameshawasilisha cheti hicho na kwamba watakipeleka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa ajili ya uhakiki.

Wakati Rais Magufuli akikabidhiwa ripoti ya uhakiki wa watumishi wenye vyeti feki alisema kuwa, kwa wale ambao wanavyeti pungufu, wanaendelee kubaki kazini lakini uhakiki ufanyike vizuri kwa sababu si kila mtu alipita kidato cha sita na kufika chuo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *