Muigizaji nyota wa Bollywood, Priyanka Chopra amewashukuru mashabiki wake waliomtakia heri kipindi alipokuwa hospitali baada ya kuumia wakati akishoot movie mpya ya ‘Quantico’ Alhamisi iliyopita.
Priyanka Chopra mwenye umri wa miaka 34 alianguka wakati wa utengenezaji wa filamu mpya ya Quantico na kusababisha kupata majeraha na kukimbizwa hospitali ili kupata matibabu.
Muigizaji huyo alitumia akaunti yake ya Twitter kuwashukuru mashabiki zake wote waliokuwa wanamuombea wakati wa kipindi hiko kigumu alichokumbana nacho lakini kwasasa anaendelea vizuri na ameruhusiwa kutoka hospitali.
Pia Muigizaji huyo amesema kuwa kutokana na hali yake kuendelea vizuri hivyo anatarajia kuendelea na utengenezaji wa filamu hiyo mpya ya ‘Quantico’.