Mwanamfalme mtawala wa Cambridge Prince William na mkewe Kate wanatarajia kupata mtoto wa tatu baada mwanamke huyo kuwa ana ujauzito.

Malkia Elizabeth na familia za wawili hao zimefurahishwa sana na taarifa hizo na kuwasili kwa mtoto wa tatu kwenye famili hiyo.

Sawa na katika mimba alizokuwa nazo awali, Bintimfalme huyo anaugua hyperemesis gravidarum, au umito.

Hataweza kutekeleza majukumu yake aliyokuwa amepangiwa kutekeleza katika kituo cha watoto cha Hornsey Road, London baadaye leo.

Mwanamfalme William na Bintimfalme Kate wana mtoto mmoja wa kiume, George, na binti mmoja, Charlotte, walio na umri wa miaka minne na miwili mtawalia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *