Mjukuu wa malkia wa Uingereza, Prince Harry amekutana mwanamuziki nyota wa Marekani, Rihana mara mbili kwa siku katika warsha ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Barbados.

Rihana ambaye muziki wake umepata umaarufu nchini Uingereza alisimama na kumsalimia Prince Harry.

Msaidizi mmoja amesema kuwa Prince Harry ambaye alivalia nguo rasmi za ufalme alisema kuwa Harrry alikuwa amejulishwa dakika 20 kabla awasili kwa warsha hiyo kuwa Rihana angehudhuria.

Baadaye Harry na Rihana tena waliketi pamoja kwenye jukwaa eneo la Kensington huko Bridgetown.

Umati wa watu 20,000 uliohudhuria ulimshangilia Prince Harry wakati jina lake lilipotajwa, Lakini kulikuwa na mbwembwe zaidi wakati jina la Rihana lilitajwa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *