Waziri wa fedha wa Afrika Kusini, Pravin Gordhan amegomea wito wa polisi nchini humo uliomtaka kuripoti kituo cha polisi na kusema kwamba tuhuma dhidi yake hazina msingi.

Waziri huyo ameeleza kuwa timu yake ya kisheria ilimshauri kutoitikia wito huo na kwamba yeye alikuwa akitimiza wajibu wake kama kawaida.

SA

Sababu ya wito huo zinatokana na uchunguzi uliofanywa dhidi ya kitengo alichowahi kukisimamaia cha masuala ya kodi ambacho kinashutumiwa kwa kuwachunguza wanasiasa nchini humo.

Upande wa upinzani unahisi kuwa waziri huyo ni mwathirika wa jaribio la kumdhoofisha linalofanywa na wafuasi wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *