Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amempongeza mpenzi wake Jux baada ya kuhitimu elimu yake ya juu nchini China.

Katika pongezi hizo Vanessa Mdee amewapiga vijembe wale waliokuwa wanamsema msanii huyo kuwa hasomi bali anakwenda kukunua nguo na kwamba picha alizoweka leo ni jibu tosha.

Vanessa Mdee  ametoa pongezi hizo ikiwa ni siku moja baada ya Msanii huyo kuhitimu na kutupia kijembe kwa wale waliokuwa wanapiga kelele siku za nyuma katika mitandao na vyombo vya habari vikimtaka Jux athibitishe kwa picha akiwa  darasani kama kweli anasoma huko, na kama jinsi wanafunzi wengine wafanyavyo wakiwa vyuoni.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Vanessa ameandika kama ifuatavyo “Congratulations Juma Jux finally done and you done did it well’. Hapo watu waliyokuwa wakiombaga picha za wewe darasani nadhani hii ni picha jibu la kutosha. Umeweza kufanya yote, muziki, biashara pamoja na shule, ‘now that’s exceptional’ muda wa vibunda baba. ‘Keep inspiring”.

Hata hivyo Jux mara nyingi amekuwa akitoa kauli ya kutothubutu kupiga picha kumuonesha akiwa darasani na kwamba yale ni maisha binafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *