Vikosi vya usalama nchini Gabon vimevamia makao makuu ya chama cha mgombea urais aliyeshindwa Jean Ping.

Bwana Ping amekiambia kituo kimoja cha redio kutoka Ufaransa RMC kwamba amekimbia mafichoni kufuatia uvamizi wa makao makuu ya chama chake usiku.

Msemaji wa serikali amesema kuwa oparesheni hiyo kwenye mji mkuu Libreville ililenga kuwafurusha wahalifu.

Alisema wao ndio walihusika katika kuchomwa kwa majengo ya bunge siku ya Jumatano.

Bwana Ping alisema kuwa watu 2 waliuawa wakati wa uvamizi katika makao makuu ya chama.

Mapema wafuasi wake waliinga barabarani kupinga tangazo kuwa rais Ali Bongo alishinda uchaguzi kwa chini ya kura 6000.

Kwa sasa kiongozi huyo wa upinzani amedai kuwa anahofia usalama wake na kwamba huenda akakamatwa muda wowote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *