Jeshi la Polisi nchini Nigeria limetahadharisha supastaa wa nchi hiyo, 2face Idibia kuwa watamtia nguvuni endapo ataendelea na mpango wake wa kuongoza maandamano kwenye mji mkuu wan chi hiyo, Lagos.

Maandamano hayo yanalenga kufikisha ujumbe kwa serikali ya nchi hiyo juu ya hali mbaya ya uchumi.

screen-shot-2017-02-03-at-14-57-16

Staa huyo ameweka wazi kuwa ni lazima serikali na watendaji wake watoe maelezo kwa wananchi juu ya sababu zinazopelekea kuanguka kwa uchumi wa nchi hiyo.

Maandamano hayo yanatarajiwa kufanyika katika miji ya Lagos na Abuja huku uhamasishaji mkubwa ukifanyika kupitia mtandaoni.

screen-shot-2017-02-03-at-14-58-35

Lakini mkuu wa Polisi wa jiji la Lagos, Fatai Owoseni amedai kuwa yeye hana taarifa za maandamano hayo na kwa taarifa za kiintelijensia walizozipata ni kuwa wahuni wanataka kuyatumia maandamano hayo kufanya uhalifu.

screen-shot-2017-02-03-at-14-57-37

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *