Jeshi la Polisi wiliyani Moshi limepiga marufuku kuutembeza mwili wa aliyekuwa mbunge wa Moshi Mjini, Phelemon Ndesamburo katika barabara za wiliaya hiyo leo.

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa na ofisi ya Polisi wilayani Moshi imezuia kupitisha mwili huo katika barabara hizo kutokana na leo kuwa siku ya kazi hivyo inaweza kusababisha msongamano wa wakazi wa Moshi.

Pia barua hiyo imebainisha kuwa wakiupitisha mwili huo barabarani utasababisha msongamano mkubwa ambao utakuwa usumbufu kwa watumiaji wa barabara.

Mwili huo wa Ndesamburo ulitakiwa kupitisha katika barabara kuu za Moshi ili kuwawezesha wananchi kuaga ambao hawatapata nafasi ya kwenda uwanja wa Majengo kwa ajili ya kuaga mwili.

Philemo Ndesamburo anatarajiwa kuzikwa kesho katika makubuli ya familia yao wilayani Moshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *