Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amepelekwa nyumbani kwake kwa ajili ya upekuzi baada ya kukamatwa jana akiwa mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Hayo yamethibitishwa na mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya nje wa Chadema , John Mrema baada ya kufika kituo cha Polisi.

Mrema amesema kuwa msafara wa magari ya Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ulielekea nyumbani kwa Lissu ambapo mawakili wa Lissu waliongozana na msafara huo.

Tundu Lissu alinyimwa dhamana jana baada ya kukamatwa kwa kosa la kumkashifu Rais Magufuli pamoja na uchochezi.

Hii ni mara ya pili jeshi la Polisi kwenda kumpekua Tundu Lissu nyumbani kwake kutokana na kesi zake za uchochezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *