Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam leo limemkabidhi mfanyabiashara, Yusuf Manji na wenzake kwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kumaliza upelelezi wao wa kumhoji katika kesi ya uhujumu uchumi.

Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi, amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi,  kuwa washtakiwa hao wamerudishwa tena Mahakamani ilivyokuwa imeamuru warudishwe baada ya Polisi kumaliza mahojiano yao.

Naye, Hakimu Shaidi aMEsema kesi hiyo itaendelea na utaratibu kama ilivyokuwa mwanzo na hivyo ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 8, mwaka huu.

Jana Mahakama hiyo iliruhusu Yusuf Manji na wenzake watatu kwenda kuhojiwa na Polisi kwa lengo la kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *