Mahakama nchini Kenya imetoa uamuzi kwamba polisi wa utawala waliwateka nyara wakili Willie Kimani, mteja wake na dereva wa texi na kuauwa, tukio ambalo lilisababisha maandamano nchini Kenya dhidi ya mauaji yanayotekelezwa na polisi.

Mahakama ya juu nchini kenya imegundua kwamba wakili Willie Kimani, mteja wake Josphat Mwenda and dereva wa texi Joseph Muiruri walitekwa nyara mwezi Juni 23 mwaka huu wakazuiliwa katika kituo cha polisi.

Mahakama hiyo pia imeamuru kwamba wakili Willie Kimani kwa sababu aliuawa na mwili wake kutupwa mtoni, atambuliwe kama mtetezi wa sheria kama njia mwafaka ya kumkumbuka.

Jaji pia alifahamu kwamba uchunguzi wa mauaji hayo uliingiliwa kati na washukiwa ambao walikuwa wamejitolea kusambaratisha haki kutendeka.

Chama cha wanasheria nchini Kenya kilikuwa kimewasilisha malalamiko mahakamani kikitaka polisi waseme wakili, mteja wake na dereva wa texi waliko wakati walipopotea.

Maafisa wanne wa polisi wa utawala tayari wameshtakiwa juu ya mauji hayo yaliyotokea mwezi juni nchini Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *