Polisi mjini Marseyside wametangaza rasmi kuanza kwa uchunguzi wa tukio la ugonvi uliotokea katika uwanja wa Goodison Park katika mchezo wa michuano ya ‘Europa League’ baina ya Everton na Lyon ambapo golikipa wa Lyon, Anthony Lopes amedai kuwa alipigwa na shabiki.

Wakati mchezo huo ukiendelea mchezaji wa Everton Ashley Williams alimsukuma mlinda mlango wa Lyon, Anthony Lopes kitendo kilichowaudhi wachezaji wa Lyon na kuanzisha ugovi amabo ulihusisha mashabiki pia.

Katika mchezo huo ambao uliisha kwa Eveton kufungwa mabao 2 kwa 1 kulionekana kikundi cha mashabiki akiwemo baba mmoja aliyekuwa na mtoto wakijaribu kutaka kuwapiga wachezaji wa Lyon pembeni mwa uwanja.

Endapo Everton watapatikana na hatia baasi watachukuliwa hatua kali haswa mlinzi wao Ashley Williams ambaye ndiye alionekana kinara katika mvutano huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *