Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema zama za watu wachache wenye fedha chafu kuhonga wanachama na kuweka viongozi wanaowataka zimekwisha.

Polepole amesema CCM sasa ni chama cha wanachama wote kama Katiba inavyosema, bila ya kujali rika wala rangi na wenye kutaka uongozi ndani ya chama kwa kutumia fedha chafu, chama hakitasita kuwachukulia hatua ikiwamo kukata majina yao.

Kiongozi huyo wa CCM aliyasema hayo mkoani Arusha alipokutana na viongozi wa chama wa Wilaya ya Arusha kutoka kata zote 25 wakiwemo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Arusha.

Aliwataka wanaCCM kuwataja viongozi wanaotaka uongozi kwa kugawa fedha chafu ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.

Polepole aliwataka wakazi wa Arusha kutorudia makosa yaliyojitokeza katika uchaguzi zilizopita.

Katibu huyo yupo mkoani Arusha kwa ziara yake ya kichama ambapo anakutana na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *