Polepole: Viongozi wa vyama vya upinzani wanawagombanisha wananchi na Serikali

0
218

Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amesema kuwa wanasiasa wa vyama vingine ambavyo siyo CCM wamekuwa na jihudi kubwa ya kuwachonganisha wananchi na kuwafitinisha na serikali.

Humphrey Polepole amesema hayo leo na kutoa wito kwa wananchi na kuwataka wawapuuze wanasiasa wanaotumia matatizo na majanga kuwa mtaji wao kisiasa kwani serikali ipo kwa ajili ya kuwahudumia.

Polepole amesema kuwa Siasa yetu ni ya Ujamaa na Kujitegemea wataendelea kuhimiza Watanzania kujitegemea na kuongeza juhudi katika kazi.

Aidha amesema mageuzi makubwa yanayoendelea ndani ya CCM yanalenga kukiimairisha Chama kuisimamia Serikali na kushughulikia matatizo ya watu.

LEAVE A REPLY