Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa anayo orodha ndefu ya viongozi wa upinzani wanaotaka kuhamia CCM.

Polepole amesema hayo jana huku akibainisha kuwa orodha hiyo inahusisha wenyeviti, madiwani na wabunge lakini siku nyingi tu alikuwa amewakatalia kuwapokea.

Hata hivyo Polepole alisema kwamba kutokana na kutuhumiwa kuwanunua sasa anafanya kweli atawachukua mmoja mmoja.

Polepole amesema amemua kuchukua uamuzi huo baada ya Chadema kuonyesha utovu wa nidhamu kwa kudai kuwa madiwani wanaokihama chama hicho wamehongwa na CCM.

Alibainisha kuwa kama chama kinakuwa na viongozi wanaoweza kuhongwa na wakahongeka basi  chama hicho kitakuwa ni cha hovyo.

Polepople amesema kuwa ‘Nilikua nakataa kuwapokea ila nina orodha kubwa wapo wenyeviti, wabunge kibao kama vile watu wanaojisaliji kodi ya majengo TRA”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *